Akamatwa akiwa na sare za Jeshi la Wananchi zenye cheo cha Luteni

0
9

Jeshi la Polisi mkoani Simiyu limemshikilia mtu mmoja aitwaye Emmanuel Mapana maarufu kama Mchambi (24), mkazi wa Mtaa wa Sima, wilayani Bariadi mkoani humo akiwa na sare za Jeshi la Wananchi zenye cheo cha Luteni.

Taarifa ya Jeshi la Polisi imesema majira ya saa 6:30 mchana leo, Kikosi Kazi cha Kupambana na Uhalifu na Wahalifu mkoani humo, kilifanikiwa kumkamata akiwa amevaa kombati ya Jeshi la Wananchi akiwa na gari aina ya Ractic, na mara baada ya kufanyiwa upekuzi, alikutwa na mkanda wa Jeshi na kompyuta mpakato moja.

Aidha, taarifa hiyo imesema Mapana alikuwa akitafutwa kwa kipindi cha muda mrefu kwa kosa la kujifanya mtumishi wa Serikali.