Mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana Taifa anashikiliwa na Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu wa Uchumi, Zanzibar (ZAECA) kwa tuhuma za kuanza kampeni za uchaguzi kabla ya wakati.
Mbali na hilo, ZAECA imesema kuwa Lulu Mwacha (29) ambaye ni Mkaazi wa Arusha anatuhumiwa kuahidi kutoa rushwa mara baada ya kupata nafasi ya ubunge wa nafasi maalum kwa kundi la vijana.
Mwacha alikamatwa Mei 17, 2020 eneo la Darajani akiwa na miadi ya kuonana na wajumbe husika, ambapo tayari mamlaka hiyo imeanza kuwahoji wahusika wote ili kuweza kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.
Tanzania inatarajiwa kufanya uchaguzi mkuu baadae mwaka huu ambapo utahusisha kuchagua rais, wabunge, madiwani na wawakilishi.