Akamatwa kwa kuigiza ana mshituko wa moyo ili asilipe bili mgahawani

0
37

Raia wa Lithunia, Aidas J mwenye umri wa miaka 50 amekamatwa nchini Uhispania kwa madai ya kuigiza amepatwa na mshtuko wa moyo katika migahawa 20 tofauti, kwa kipindi cha mwaka mmoja ili kukwepa kulipa bili zake.

Katika ulaghai wa hivi majuzi, Aidas aliagiza chakula na chupa mbili za vileo zenye thamani ya TZS 92,000 katika mgahawa wa El Buen Comer huko Alicante, baada ya kumaliza mlo wake inasemekana mwanaume huyo alijaribu kuondoka bila kulipa. Alipokabiliwa na wafanyakazi wa mgahawa huo alidai anakwenda kuchukua pesa kwenye chumba chake cha hoteli ili aweze kulipa bili yake lakini hawakukubaliana naye.

Baada ya kukataliwa, kwa mtindo wa kushangaza alijifanya amepatwa na mshituko wa moyo akaanguka chini na kisha akajifanya amezirai huku akijilaza sakafuni.

Watatu wafariki, polisi ajeruhiwa kwenye vurugu za kutoa uchawi

Badala ya kupigia gari la wagonjwa, meneja wa mgahawa huo aliwapigia simu polisi wa eneo hilo ambao waliweza kumtambua mtu huyo kwa urahisi kutokana na ulaghai wake wa awali wa mshituko wa moyo.

Tapeli huyo amefungwa kwa muda wa siku 42 baada ya kukataa kulipa faini mbili alizotozwa kutokana na vitendo vyake vya udanganyifu lakini wamiliki wa hoteli alizolaghai wanataka apewe kifungo cha muda mrefu zaidi.

Send this to a friend