Akamatwa kwa kujaribu kukata sehemu za siri za dereva teksi

0
38

Mwanaume mmoja huko Chimoio katikati mwa Msumbiji, anashikiliwa na Polisi baada ya kukiri kujaribu kukata sehemu za siri za dereva wa teksi.

Mshukiwa huyo aliwaambia maafisa wa Polisi kuwa alijifanya mteja ili kumrubuni dereva wa teksi hadi msituni, ambapo akiwa na mwenzake walimvamia mwathiriwa kwa kutumia vifaa butu.

Aidha, mshukiwa ambaye jina lake halikutajwa, anasema anajuta na anakusudia kusaidia Polisi kumsaka mpenzi wake ambaye amekimbia.

Hata hivyo, haijulikani ni kwa nini dereva wa teksi alilengwa, lakini taarifa zinasema wanaume wenye vipara hapo awali walilengwa na watu wanaotaka kutumia viungo vyao vya mwili kwa ajili ya matambiko.

Send this to a friend