Akamatwa kwa kuwatukana viongozi wakuu wa Serikali mtandaoni

0
34

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia mtu mmoja  anayejulikana kwa jina la Selemani Hagayi mkazi wa Kigamboni kwa tuhuma za kuwatukana viongozi wakuu wa serikali kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi, Jumanne Muliro amesema Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo Julai 29, mwaka huu baada ya kumfatilia kwa kutumia mfumo wa TEHAMA.

“Tumemkamata baada ya kubainika yeye pamoja na wenzake walitengeneza video zilizokuwa zinawatukana viongozi wakuu wa Serikali kisha kuzisambaza katika mitandao ya kijamii.

Mahakama yaamuru nyumba iuzwe kulipa deni la mahari

“Mtandao ambao walitumia kusambaza video hizo ni TikTok. Mtuhumiwa huyo tayari ameshahojiwa kwa kina na atafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo,” amesema.

Aidha, Jeshi la Polisi limetoa onyo kwa watu wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya na kwamba watu hao watachukuliwa hatua mara moja ili iwe fundisho kwa watu wengine.

Send this to a friend