Akamatwa kwa madai ya kuponya UKIMWI kwa kitunguu

0
40

Mtu mmoja nchini Uganda anayejulikana kwa jina la Dkt. David Ssali amekamatwa na polisi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Kitaifa ya Dawa (NDA) kwa tuhuma za kueneza habari za kupotosha  ikiwa ni pamoja na madai ya kuponya virusi vya UKIMWI kwa vitunguu.

Akizungumza msemaji wa NDA, Abiaz Rwamwiri amesema kukamatwa kwa mtu huyo ni kutokana na malalamiko ya watu wengi pamoja na taarifa nyingine za kijasusi zilizokusanywa na Shirika la Kupambana na Dawa za Kulevya na Polisi.

“Mtu huyu  amekuwa akitumia mitandao ya kijamii, hasa TikTok kinyume cha sheria kwa muda kutangaza dawa za kulevya na kutoa madai ya kupotosha kuhusu matibabu na tiba, ikiwa ni pamoja na kuponya VVU/UKIMWI kwa vitunguu,” amesema Rwamwiri.

“Hii inakiuka sheria ya NDA na miongozo mingine ya afya ya umma. Baada ya kukusanya taarifa zetu za kijasusi, tulishirikiana na polisi na kumkamata,” ameongeza.

Kinywaji cha ‘kuongeza’ nguvu za kiume chapigwa marufuku

Mbali na hayo, amebainisha kuwa Dkt. Ssali aliendesha zahanati kinyume cha sheria katika mazingira hatarishi pamoja na kubainika kuuza zaidi ya bidhaa 20 ambazo hazikuwa na leseni.

Katika mojawapo ya video za TikTok, Dk. Ssali ameonesha mteja wake anayeishi China ambaye ameponywa UKIMWI kwa kutumia kirutubisho cha kitunguu alichoagiza, kitendo kilichochukuliwa kama upotoshaji ambao unaweza kusababisha matatizo ya kiafya na hata kusababisha kifo.

Send this to a friend