Akamatwa kwa madai ya kuua watu wawili Kigamboni

0
48

Jeshi la Polisi Kanda Maalim Dar es Salaam linamshikilia Mohamed Jumaa (37), mkazi wa Kariakoo kwa tuhuma za mauaji ya watu wawili na kujeruhi wengine sita.

Jumma anatuhumiwa kuwaua kwa kuwagonga kwa gari Eliakim Morali (30), mkazi wa Mbezi Beach na Mlinzi wa Kampuni ya Lock Fort Security na Saunkoo Bakari (35), mkazi wa Buguruni ambaye alikuwa mlinzi binafsi (baunsa).

Taarifa ya polisi imeeleza kuwa Agosti 26, 2021 majira ya saa 12 jioni eneo la Tungi wilayani Kigamboni mkoani Dar es Salaam katika kituo cha kuuzia mafuta cha JM Petrol Station mtuhumiwa aliwaua kwa makusudi walinzi hao kwa kuwagonga na gari (T176 CVP) aina ya DAF lori

Mtuhumiwa alifika katika kituo hicho cha kuuzia mafuta alichokuwa anakimiliki kwa ajili ya kuhamisha mali zake, lakini alichukua gari lake na kutoka nje ya kituo na ghafla alirudi nalo kwa kasi na kuwagonga walinzi hao waliokuwa getini na kupelekea kufariki dunia papo hapo, na kuwajeruhi watu sita ambao walikimbizwa hospitalini kwa matibabu.

Mtuhumiwa huyo alikuwa na kesi ya madai namba 118/2018 mahakama kuu iliyofunguliwa na Access Benki baada ya kushindwa kulipa mkopo kwa muda muafaka aliochukua katika benki hiyo na mtuhumiwa alishindwa mahakamani licha ya kukata rufaa mara kadhaa na hatimaye mahakama ilitoa amri ya kuuzwa kwa kituo hicho.

Send this to a friend