Akataa kutoka gerezani baada ya mahakama kumwachia huru

0
26

Kiongozi wa dini ya Kiislamu, Sheikh Guyo Gorsa Buru ameiomba kutoka nchini Kenya ameng’ang’ania kubaki gerezani licha ya mahakama kumwachia huru katika kesi ya ugaidi iliyokuwa ikimkabili.

Kiongozi huyo amekataa kuondoka katika gereza maarufu la Kamiti akisema anahofia maisha yake huku akidai kuwa anaweza kutekwa nyara na kuuawa na serikali mara tu atakapokuwa uraiani

Sheikh Buru alikamatwa Januari 2018 huko Marsabit Kaskazini mwa Kenya na kushtakiwa kwa kujihusisha na kundi la kigaidi kwa kushirikiana na kundi la wanamgambo wa Al-Shabab.

Hata hivyo Hakimu aliamuru akae gerezani kwa muda usiozidi siku 30 kisha aachiwe huru.

Send this to a friend