Akaunti ya YouTube ya Diamond Platnumz yafungwa

0
58

Akaunti ya YouTube ya mwanamuziki maarufu kutoka Tanzania, Diamond Platnumz imefungwa kwa kukiuka utaratibu na masharti ya mtandao huo.

Platnumz ambaye jina lake halisi ni Naseeb Abdul alikuwa na wafuasi zaidi ya milioni 6 kwenye akaunti hiyo, ikiwa na video ambazo kwa ujumla zimetazwa zaidi ya mara bilioni 1.

Mtandao wa YouTube umeeleza kuwa akaunti hiyo imefungwa kutokana na kukiuka masharti na sheria zake.

Shaban Tale Tale, maarufu Babu Tale ambaye ni meneja wa msanii huyo akizungumzia sakata hilo amesema kwamba akaunti hiyo imedukuliwa, tukio ambalo limejirudia kwa mara ya pili.

Bosi huyo wa WCB hajazungumza chochote kuhusu tukio hilo.

Send this to a friend