Akiri kutengeneza dawa feki za kulevya na kusafirisha kwenye mabasi mikoani

0
62

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) inamshikilia Shaban Adam (54) mkazi wa jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kutengeneza dawa feki za kulevya aina ya heroini.

Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretas Lyimo amesema baada ya mtuhumiwa huyo kuhojiwa alikiri kutengeneza dawa hizo, na kueleza kwamba huzisafirisha dawa hizo kwa kutumia mabasi ya abiria kama vifurushi kwenda mikoa mbalimbali nchini.

“Ameieleza mamlaka kuwa, siku za nyuma alikuwa akitengeneza dawa hizo za kulevya katika nchi za bara la Asia kwenye magenge ya wazalishaji wa dawa za kulevya na alitumika kama mbebaji wa dawa hizo (punda) na aliporejea hapa chini aliendelea na uhalifu huo,” amesema.

Ameongeza kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa nyumbani kwake Manzese Kilimani Juni 11, mwaka huu akitengeneza dawa za kulevya alizozitambulisha kama heroini kwa kutumia dawa tiba zenye asili ya kulevya akichanganya na kemikali bashirifu.

Send this to a friend