Alama 5 zitakazokuonesha kama bidhaa ni feki au halisi

0
43

Bidhaa za kughushi zimekuwa zikienea kila mahali na kupelekea watu kununua bidhaa zisizofaa na hata kuleta madhara ya kiafya. Hakuna anayetaka kulaghaiwa kununua bidhaa isiyo halisi. Hivyo angalia orodha hii kabla ya kwenda kununua kitu ili kuepuka kununua kitu cha bandia.

Bei ya bidhaa
Iwe unafanya manunuzi dukani au mtandaoni, bei inaweza kuwa mojawapo ya viashirio vya kwanza kuonesha bidhaa ni bandia. Mara nyingi bei hupungua sana kutokana na bidhaa kuwa duni. Ni vyema kuwa makini endapo bidhaa unayotaka kununua ina punguzo la bei ya chini kuliko kawaida kwani wazalishaji wake hupenda kuvutia umakini wa watu kwa bei zisizo halisi.

Ubora
Bidhaa za kughushi mara nyingi huzalishwa kwa kutumia vifaa vya bei nafuu (materials) na visivyo na ubora kama vile ngozi bandia, glasi ya ubora wa chini, vifaa vya nguo duni au zilizotumika. Ikiwa bidhaa haionekani kuwa halisi, kuna uwezekano sivyo. Wauzaji bidhaa wanaoheshimika wanapaswa kuwa na taratibu za ukaguzi na uthibitishaji pamoja na mafundi kukagua ubora wa bidhaa wanazouza. Epuka kununua bidhaa zenye maneno ya kuvutia kama ‘real’, ‘authentic’, ‘kali’, ‘mpya’, ‘Royal’ n.k.

Vifungashio
Kukagua vifungashio ni njia nyingine ya kutofautisha bidhaa asili na bandia. Biashara zinazotambulika huwekeza katika vifungashio vyenye ubora wa juu kwa hivyo ukipokea bidhaa katika vifungashio vya kutiliwa shaka, au zikiwa zimefungwa kwenye kile kinachoonekana kuwa cha bei nafuu basi inaweza kuwa ishara mbaya.
Vile vile, jihadhari na vifungashio ambavyo muda wa matumizi ‘tarehe’ imepita, vimevunjika, kukosa mihuri ya usalama, au vinakosa maelezo ya udhamini au maelezo ya mawasiliano ya mtayarishaji.

Nani anaiuza?
Kampuni nyingi au chapa zinaorodhesha wauzaji wao walioidhinishwa kwenye tovuti yao au ndani ya vifaa vya ufungaji. Kampuni hutoa orodha ya wauzaji wa rejareja walioidhinishwa kwa kubandika katika URL ya tovuti, ili watumiaji waweza kuangalia. Ikiwa una shaka kuhusu chanzo cha bidhaa basi muulize muuzaji kuhusu msambazaji wake.

Tiba rahisi ya kutengeneza nyumbani ya kuondoa weusi kwenye makwama

Njia ya malipo
Kwa ununuzi wa mtandaoni, hakikisha kwamba malipo yako yamewasilishwa kupitia tovuti zinazoanza na https:// na ambazo zinaambatana na alama ya kufuli. Wauzaji halali wa mtandaoni huwa na tabia ya kuomba malipo kupitia kadi za mkopo au benki, au kwa PayPal kwa hivyo watumiaji wanapaswa kuwa na shaka wakiombwa kufanya malipo kupitia uhamishaji wa pesa wa moja kwa moja, kama vile uhamishaji wa benki

Send this to a friend