Albamu 10 za Hip-hop zilizouzwa zaidi ulimwenguni

0
95

Muziki wa Hip-Hop ulianza kuwa maarufu katika miaka ya 1980 na 1990 kama muziki wa rap. MaDJ waanzilishi wa hip-hop ni pamoja na Kool Herc, Grandmaster Flash, na Afrika Bambaataa.

Mpaka sasa umekuwa ni miongoni mwa aina ya muziki unaosikilizwa na kupendwa ulimwenguni.

Hii ni orodha ya albamu za Hip-hop zilizouza nakala nyingi zaidi ulimwenguni;

Illmatic – Nas (1994)

Albamu ilipata nafasi ya 12 kwenye chati ya Billboard 200 ya Marekani, na kuuza nakala 63,000 katika wiki yake ya kwanza. Mnamo Desemba 11, 2001, ilipata cheti cha platinamu baada ya kusafirisha nakala 1,000,000 nchini Marekani. Kufikia Februari 6, 2019, albamu hiyo ilikuwa imeuza nakala milioni 2 nchini Marekani.

2Pac – All Eyez On Me (1996)

All Eyez on Me ni albamu ya mwisho iliyotolewa wakati wa uhai wa 2Pac. Albamu ilitajwa namba moja kwenye Billboard 200 kama albamu bora za R&B/Hip-hop pamoja na kupata tuzo ikiwemo tuzo ya Soul Train Music kwa Albamu ya Rap ya Mwaka. Zaidi ya nakala milioni kumi zimeuzwa kote ulimwenguni.

The Notorious BIG – Life After Death (1997)

Amerika ilimpoteza rapper na mtunzi mahiri wa nyimbo. Mara nyingi anafananishwa na 2Pac kama mmoja wa wasanii bora wa Hip-hop. Wiki mbili baada ya mauaji ya Biggie mnamo Machi 9, 1997, albamu yake ya Life After Death ilitolewa na zaidi ya nakala milioni kumi zimeuzwa.

Outkast – Speakerboxx/The Love Below (2003)

Outkast walikuwa wana hip-hop wawili, Andre 3000 na Big Boi wa Kimarekani walioanza rasmi mwaka 1992. Wawili hao ni miongoni mwa wasanii wa hip-hop wenye ushawishi ulimwenguni.

Ikiwa na zaidi ya nakala 510k kuuzwa katika wiki yake ya kwanza, albamu iligonga moja kwa moja kwenye Billboard 200 na kuchukua Albamu Bora ya Mwaka na Albamu Bora ya Rap katika tuzo za 46 za kila Mwaka za Grammy.

Orodha 10 ya wasanii Afrika wanaotazamwa sana Youtube

Eminem – The Marshall Mathers LP (2000)

Mafanikio ya Eminem yamekuwa sababu kuu katika kupunguza ubaguzi wa rangi katika tasnia ya hip-hop. Zaidi ya nakala milioni 25 za albamu hiyo zimeuzwa hadi sasa, na kupata hadhi ya platinamu 11 na Chama cha Recording Industry Association of America (RIAA).

Beastie Boys – Licensed To Ill (1986)

Nchini Marekani, kundi la rap la Beastie Boys lilionekana kwa mara ya kwanza mwaka wa 1981. Walikuwa kundi la rap lililouza zaidi tangu Billboard ilipoanza kuweka rekodi za mauzo mwaka wa 1991, na waliingizwa kwenye Rock and Roll Hall of Fame mwaka wa 2012. Albamu imeuza zaidi ya nakala milioni 10 duniani kote.

Lauryn Hill – The Miseducation Of Lauryn Hill (1998)

Hill alivunja rekodi ya mauzo bora ya albamu ya wiki ya kwanza na msanii wa kike katika karne ya 20. Albamu hiyo iliongoza kwenye Billboard 200 ya Marekani, nafasi ambayo haijawahi kushuhudiwa kwenye chati kwa rapa wa kike. Zaidi ya nakala milioni ishirini zimeuzwa.

Nyimbo za Tanzania zinazotazamwa sana Youtube kuanzia mwezi Februari 2023

Nelly –  Country Grammar (2000)

Albamu ya kwanza ya Nelly, Country Grammar iliidhinishwa kuwa Diamond na Chama cha Recording Industry Association of America (RIAA) mwaka wa 2016. Rekodi hiyo ilitolewa awali Juni 27, 2000 na ilibaki nambari moja kwenye chati ya Billboard ya Marekani kwa jumla ya wiki tano mfululizo na tangu kuachiliwa kwake, albamu hiyo imeuza nakala zaidi ya milioni kumi.

MC Hammer – Please Hammer Don’t Hurt ‘Em (1990)

Please Hammer Don’t hurt ‘Em ni albamu yake ya tatu  na yenye mafanikio zaidi hadi sasa, ilitawala chati ya albamu za juu za R&B/Hip-Hop kwa jumla ya wiki 28 na ilitumia wiki 21 ikiwa kileleni mwa Billboard 200 za Marekani. Albamu  hii iliuzwa zaidi mwaka wa 1990 nchini Marekani na ina nakala milioni 17 duniani kote.

Eminem – The Eminem Show (2002)

Albamu zake zimeorodheshwa kati ya albamu za rap zinazouzwa zaidi. Kipengele kingine kinachompa umaarufu ni kwamba yeye ni rapa wa kizungu, na sote tunajua Waamerika wa Kiafrika wanatawala tasnia ya rap. Kulingana na Live About, albamu hiyo ilipaswa kutolewa mnamo Juni 2002, lakini ilitolewa Mei 2002 na nakala zaidi ya milioni ishirini zimeuzwa.

Send this to a friend