Alichoandika Bernard Morrison baada ya taarifa ya Simba SC

1
77

Winga wa Simba SC, Bernard Morrison ameeleza kwamba anasikitika kukosa sehemu ya msimu iliyosalia kwani analazimika kuwa nje ya uwanja kutokana na sababu za kifamilia zilizo nje ya uwezo wake.

Morrison ambaye amekuwa mchezaji mwenye mchango mkubwa kwenye klabu hiyo amesema imemlazimu kuchukua hatua hiyo kwani ushiriki wake unaweza kuathiri ufanisi wa timu.

“Mengi yanahitaji kusemwa kuhusu hilo, lakini niitakie klabu kila la heri [tafsiri ya mwandishi],” ameandika Morrison dakika chache baada ya taarifa rasmi ya klabu.

Simba imesema Morrison amekuwa na mchango wa kuiwezesha kufika robo fainali ya michuano ya Afrika mara mbili, kuchukua ubingwa wa ligi Tanzania Bara na kombe la shirikisho nchini na kombe la Mapinduzi.

“Simba inamtakia kila la heri Bernard Morrison katika mapumziko yake na safari yake ya soka hapo baadaye,” imeeleza Simba.

Morrison alijiunga Simba SC misimu miwili iliyopita akitokea kwa watani wa jadi Yanga SC.