Alichosema Khadija Kopa kuhusu uhusiano wa Diamond na Zuchu

0
105

Mwanamuziki Khadija Khopa ambaye pia ni mama wa msanii Zuhura Othman Soud ‘Zuchu’ amesema haoni ajabu kwa mwanaye kuitwa mke na msanii ambaye pia ni boss wake, Naseeb Abdul ‘Diamond’ kwa kuwa huenda msanii huyo anaiona kesho yake na binti yake.

Hayo yamekuja siku kadhaa baada ya msanii Diamond kuweka wazi kile kinachoaminiwa kuwa ni uhusiano wake na Zuchu na kumwita mke, huku pia mama mzazi wa Diamond akimwita mkwe wakati akimtakia tamasha jema Zuchu nchini Marekani.

“Sioni shida mama Diamond kumwita Zuchu mkwe kwa sababu ana mtoto wa kiume, pia sishangai Diamond kumwita Zuchu mkewe inawezekana anaiona kesho yake njema na binti yangu,” amesema Khadija.

Akizungumzia kuhusu suala la posa, iwapo familia ya Diamond imekwishatoa kwa ajili ya binti yake mama huyo amesema suala hilo bado halijafanyika ila wakati ukifika kila kitu kitakuwa wazi.

Amefafanua kuwa binti yake huitwa mkwe kila upande na wala hajui atakayemuoa kwa kuwa amekuwa ‘mkwe wa taifa’ kutokana na yeye kuwa maarufu pia ni mtoto wa kike.

Chanzo: Mwananchi

Send this to a friend