Alichosema Nugaz baada ya kuondoka Yanga

0
43

Saa chache baada ya Yanga kutangaza kutomwongezea mkataba, aliyekuwa afisa mhamasishaji wa klabu hiyo, Antonio Nugaz ameushukuru uongozi wa klabu hiyo kwa nafasi waliyompa kwa miaka miwili na kuwatakia heri kuiongoza klabu hiyo.

“Kwa udhati wa Moyo wangu naomba niwashukuru Kuanzia Uongozi wote wa Yanga chini ya mwenyekiti wetu Dk. Mshindo Mbette Msolla na Kaimu Katibu Mkuu Mpya Senzo Mbatha Mazingiza, wafanyakazi wenzangu wote kwa upendo wenu kwa kipindi chote cha miaka miwili niliyoitumikia @yangasc kwa moyo Mkunjufu na kujitoa kwangu, Mungu awabarik, awalinde na awape kila hitajio la nafsi zenu ili tuweze kuipeleka mbele Brand ya Yanga.”

Amewashukuru pia wanachama, wapenzi na mashabiki wa Yanga kwani wamekuwa naye kwa moyo mmoja na kwamba anawapenda sana na ataendelea kuwa nao.

Send this to a friend