Alichosema Tundu Lissu baada ya kufika Ubelgiji

0
47

Aliyekuwa mgombea Urais wa Tanzania, Tundu Lissu amesema alichagua kwenda Ubelgiji kwa sababu ana kibali cha mkaazi, hivyo ilikuwa rahisi kwake kwenda huko kuliko nchi nyingine.

Akizungumza na BBC kuhusu sababu ya kuondoka nchini kwenda Ubelgiji, Lissu amesema hajaomba hifadhi hivyo yeye si mkimbizi wa kisiasa kwani ana kibali cha ukaazi nchini Ubelgiji, sehemu alipokaa kwa takribani miaka mitatu akipatiwa matibabu.

Lissu aliondoka nchini Novemba 10 mwaka huu akitokeka katika makazi ya Balozi wa Ujerumani alimokimbilia kwa madai kuwa ametishiwa maisha.

Mwanasaisa huyo amesema kuwa ulinzi aliokuwa amepewa wakati wa kampeni uliondolewa mara baada ya matokeo ya uchaguzi kutolewa, na muda mfupi baada ya hapo akaanza kupokea vitisho kutoka kwa watu ambao amesema hawajui.

Aidha, amesema ni kawaida kwa wanasiasa kukimbilia kwenye nchi nyingine pindi wanaopoona kuwa uhai wao upo mashakani kutokana na shughuli zao za kisiasa.

Serikali ya Tanzania imetupilia mbali madai hayo na kusema kuwa wanasiasa wa upinzani wamekuwa wakiyatoa kila mara wanaposhindwa uchaguzi.

Send this to a friend