Aliyeacha kitambulisho Muhimbili kama dhamana ya deni milioni 9 asamehewa

0
57

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amemtaka Mwanafunzi wa Chuo cha Serikali za Mitaa (LGTI) Hombolo, Dodoma, Lightness Shirima kufika Hospitali ya Taifa Mhumbili-Mloganzila na kuonana na mkurugenzi wa hospitali hiyo kesho Agosti 09, 2022 kuchukua kitambulisho chake.

Ameyasema hayo baada ya msichana huyo kuripotiwa na chombo kimoja cha habari kuwa anadaiwa TZS milioni 9, deni ambalo aliliacha baba yake baada ya kufariki dunia katika hospitali hiyo, hivyo kuacha kitambulisho chake cha NIDA kama dhamana.

Waziri Ummy amesema Serikali ya Rais Samia Suluhu inatambua kuwa wananchi wengi hawawezi kumudu gharama za matibabu hususani katika kipindi ambacho matibabu yana gharama kubwa, hivyo Serikali inakuja na Sheria ya Bima ya Afya kwa kila Mtu (UHC) ili kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma za afya bila ya kikwazo cha fedha.

Send this to a friend