Aliyefumua kidonda cha mgonjwa kwa kushindwa kulipia asimamishwa kazi

0
43

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Wizara ya TAMISEMI zimefanikiwa kumpata mhudumu wa afya aliyetoa nyuzi kwenye kidonda cha mgonjwa baada ya kushindwa kulipa gharama za matibabu.

https://swahilitimes.co.tz/2021/09/asakwa-kwa-kumfumua-mgonjwa-kidonda-baada-ya-kushindwa-kulipia/

Kupitia ukurasa wa Instagram TAMISEMI imeeleza kuwa tukio hilo lilitokea Julai, 2021 na mtumishi aliyekiuka miiko ya udaktari anaitwa Jackson Meli ambaye ni Afisa Tabibu (Clinical Officer) wa Kituo cha Afya Kerenge, Tarafa ya Magoma, Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.

Taarifa ya wizara imeeleza zaidi kuwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo ameshachukua hatua kwa kumsimamisha kazi na amempa hati ya mashtaka. Aidha, ameshafikishwa kwenye baraza la taaluma ili achukuliwe hatua stahiki kwa kwenda kinyume na miiko ya taaluma ya udakrari.

Send this to a friend