Aliyekuwa akitumia hirizi kuwakimbia Polisi akamatwa

0
80

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amesema wanawashikilia watu 10 kwa tuhuma mbalimbali za uhalifu akiwemo mtuhumiwa mmoja anayedaiwa kutumia hirizi akiamini hatakamatwa na polisi huku akitumia funguo bandia kufungua milango.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda Bukumbi ameeleza Emmanuel Hassan anayetuhumiwa kuvunja nyumba za watu, alinaswa eneo la Mashine Tatu akijaribu kuwakimbia polisi kwa madai kuwa hirizi yake ilimpa taarifa.

Kamanda amesema mtuhumiwa aliificha hirizi yake kwenye pochi ya kuhifadhia fedha, katika mfuko wa nyuma wa suruali, na kudai hirizi hiyo huvimba kama ishara ya hatari.

Hata hivyo Kamanda ameeleza kuwa hirizi imechomwa lakini haijaungua.