Aliyekuwa bosi TRA na wenzake wahukumiwa kulipa bilioni 1.5

0
49

Mahakama ya Uhujumu Uchumi nchini Tanzania imewahukumu aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Harry Kitillya, Shose Sinare, Sioi Solomon, Bedason Shallanda na Alfred Misana kulipa fidia TZS 1.5 bilioni kwa kuisababishia hasara Serikali na kila mmoja kulipa faini shilingi milioni 1 ya mahakama au kwenda jela miezi 6, kutoka na kesi ya Uhujumu Uchumi iliyokuwa inawakabili.

Mahakama imetoa adhabu huyo baada ya washtakiwa hao kukiri kosa lililokuwa likiwakabili la kuisababishira serikali hasara.

Kesi ya washtakiwa hao ambao wamesota rumande tangu mwaka 2016 ilianza kusikiliwa jana jioni na kumalizika saa 2 usiku.

Washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na kashfa ya udanganyifu wa riba ya mkopo wa Dola za Kimarekani milioni 600 ambazo zilikopwa na serikali ya Tanzania kutoka kwa benki ya Standard ya Uingereza.

Benki ya Standard ilikubali kuipokesha Serikali ya Tanzania kiasi hicho cha fedha kwa makubaliano ya riba ya asilimia 1.4, lakini Benki ya Stanbic, tawi la Tanzania iliongeza asilimia moja na hivyo kufanya serikali kutakiwa kulipa riba ya asilimia 2.4.

Send this to a friend