Aliyekuwa bosi wa Bohari ya Dawa na msaidizi wake washikiliwa na TAKUKURU

0
42

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) inamshikilia aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Bohari ya Dawa Tanzania (MSD), Laurian Bwanakunu kwa tuhuma za rushwa.

Pamoja na Bwanakunu, TAKUKURU inamshikilia pia Kaimu Mkurugenzi wa Lojistiki wa MSD, Byekwaso Tabura kwa lengo la kupisha uchunguzi.

Wawili hao wanatuhumiwa kutenda makosa ya matumizi mabaya ya madaraka pamoja na kuisababishia serikali hasara kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya mwaka 2007.

Wawili hao wapo mahabusu katika ofisi za TAKUKURU zilizopo Upanga jijini Dar es Salaam kuanzia leo Juni 2, 2020.

Send this to a friend