Aliyekuwa bosi wa TPA, Eric Hamissi arejeshwa MSCL

0
79

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Eric Benedict Hamissi kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL).

Kabla ya uteuzi huo Hamissi alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

Aidha, Rais Samia amemteua Stephen Kagaigai kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Kagaigai anachukua nafasi ya Balozi Herbert Mrango ambaye amemaliza kipindi chake.

Awali, Erick Hamissi alikuwa Mkurugenzi wa Kapuni ya Huduma za Meli (MSCL) na baadaye akateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) ambapo alichukua nafasi ya Eng. Deusdedith Kakoko kabla ya kurudishwa MSCL.