Aliyekuwa Meya wa Ilala amuomba radhi Dkt. Magufuli kwa kumhujumu akiwa UKAWA

0
46

Aliyekuwa Diwani wa Vingunguti na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Omar Kumbilamoto amemuomba radhi Dkt. John Magufuli kwa kuihujumu serikali wakati akiwa upinzani (UKAWA).

Akizungumza leo katika mkutano wa kampeni wa mgobmbea huyo wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika Kinyerezi, Dar es Salaam, Kumbilamoto amewaomba radhi pia waliokuwa viongozi wa mkoa na wilaya hiyo pamoja na wananchi.

“Ninaomba msamaha kwa mabaya niliyowafanyia nikiwa upinzani,” amesema huku akitaja miradi ambao walikataa kuitekeleza akiwa UKAWA kwani waliona kufanya hivyo ni sawa na kumuinua Rais Magufuli.

Amesema miradi waliyoikwamisha ni pamoja ujenzi wa daraja la Ulongoni, machinjio ya Vingunguti  na miradi ya kuboresha miundombinu ya jiji la Dar es Salaam (DMDP).

Ameongozeza kuwa baada ya Manispaa ya Ilala kurudi CCM, miradi hiyo inatekelezwa ambapo baadhi tayari imekamilika.

Kumbilamoto alikuwa diwani kupitia Chama cha Wananchi (CUF) kabla ya kujiuzulu na kujiunga Chama cha Mapunduzi (CCM) mwaka 2018 ambapo aligombea tena na kufanikiwa kuchaguliwa kuwa diwani.

Send this to a friend