Aliyekuwa mtia nia ya Urais Uganda afungwa jela miaka mitatu

0
43

Mahakama ya Juu nchini Uganda imemhukumu aliyekuwa mtia nia ya kugombea Urais nchini humo kwa kutumia lugha ya matusi dhidi ya majaji wa mahakama hiyo.

Ivan Samuel Ssebadduka amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela ambapo amekutwa na hatia ya kuwaita majaji hao wapumbavu wasio na uwezo.

Mtia nia huyo alifungua kesi mahakamani hapo akiitaka mahakama hiyo kusitisha utaratibu wa watia nia ya kugombea urais kukusanya saini za wadhamini kama kigezo cha kutaeuliwa kugombea.

Aidha, aliitaka mahakama hiyo isitishe kanuni za kiafya za kukabiliana na virusi vya corona zilizotolewa na wizara ya afya wakati wa mikutano ya kampeni.

Ssebadduka alitumia lugha ya matusi dhidi ya majaji hao wakati akitoa utetezi katika kesi hiyo.

Jaji Mkuu, Alfonse Owinyi-Dollo amesema ukosoaji dhidi ya majaji unatakiwa kuwa sahihi na wa haki na hautakiwi kukiuka haki za wengine.

Send this to a friend