Aliyekuwa Rais wa Afghanistan aomba radhi kwa kukimbia nchi

0
37

Aliyekuwa Rais wa Afghanistan, Ashraf Ghani ameomba msamaha kwa watu wa Afghanistan baada ya kukimbilia katika nchi za Falme za Kiarabu kufuatia mapinduzi yaliyofanya na Talibani.

Amesema maafisa usalama wa Rais ndio waliomshaui kuondoka ili kuinusuru nchini hiyo kwa maipgano, na kwamba kama angesalia, huenda mapigano zaidi yangezuka.

Ghani aliikimbia nchi hiyo wakati wanamgambo wa Taliban walipokuwa wakiendelea kuingia kwenye mji mkuu, Kabul Agosti 15 mwaka huu., ikiwa hatua ya mwisho ya kuipindua serikali.

“Kuondoka Kabul ulikuwa uamuzi mgumu zaidi maishani mwangu. Ilikuwa ndio njia pekee iliyosalia,” amesema kiongozi huyo na

Ameleza kusikitishwa na namna uongozi wake wa miaka 20 wenye lengo la kurejesha demokrasia nchini humo ulivyoisha kwa majuto kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake.

Send this to a friend