Mfanyabiashara Kaloli Mkusa (30) mkazi wa kijiji cha Msisina, amehukumiwa na mahakama ya Wilaya ya Iringa kifungo cha miaka 30 na fidia ya TZS milioni 1 kwa kosa la kumbaka mama yake Mzazi.
Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo, Emmy Msangalufu amesema mtuhumiwa alifanya tukio hilo Mei 07 mwaka huu ambapo siku ya tukio alikwenda nyumbani kwa mama yake usiku na kuvunja mlango huku akiwa ameshika panga na kumtisha kumkata kwa kumpiga na ubapa wa upanga hilo.
Licha ya mama yake kumsihi asifanye hivyo lakini mtuhumiwa aliendelea na kumbaka mama yake mpaka alipomaliza, baada ya tukio mama alitoa taarifa kwa majirani kisha Serikali ya Kijiji na ndipo taratibu za kumkamata zikafanyika.
Aidha, inadaiwa kuwa tukio hilo linasadikiwa linatokana na imani za kishirikina kutokana na biashara ya mtuhumiwa kuyumba, mtuhumiwa alikuwa akifanya biashara zake Tunduma mkoani Songwe na alirudi nyumbani akifikia kwa baba yake ambaye alitengana na mama yake na kupeana talaka.
Hati ya kukamatwa ilitolewa Machi 9 mwaka huu lakini mpaka sasa mtuhumiwa pamoja na baba yake aliyemuwekea dhamani hawajulikani walipo, na kwa mujibu wa Mahakama kifungo hicho kitaanza kutumika pindi mtuhumiwa huyo atakapokamatwa.