Aliyemtapeli Ridhiwani Kikwete milioni 4 aenda jela miaka saba

0
57

Innocent Chengula (23), kijana anayedaiwa kumtapeli Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti na Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amehukumiwa kwenda jela miaka saba baada ya kupatikana na hatia ya kosa hilo.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam baada ya kupatikana na makosa sita likiwamo la kujipatia TZS milioni 4 kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa kiongozi huyo.

Kijana huyo mkazi wa Kigogo Luhanga, alijipatia pesa hizo baada ya kujitambulisha kwa Ridhiwani kuwa yeye ni Dkt. Hassan Abbas, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii kwa sasa, ambapo mahakama hiyo imeamuru kumlipa Ridhiwani kiasi cha shilingi milioni 4, anachodaiwa kumtapeli.

Mbali na adhabu hiyo, Mahakama imetaifisha simu moja ya mkononi pamoja na laini tatu za simu alizokuwa akitumia mshtakiwa huyo kufanya udanganyifu katika mitandao ya kijamii akijivika wadhifa wa viongozi nchini.

Send this to a friend