Aliyetoroka gerezani Afrika Kusini akamatwa Tanzania

0
39

Jeshi la Polisi nchini limethibitisha kuwakamata raia watatu wa Afrika Kusini ambao ni Thabo Bester maarufu kwa jina la ‘Mbakaji wa Facebook’, Mpenzi wake Dkt. Nandipa Magumana na Zakaria Alberto.

Msemaji wa Polisi, SACP David Misime amesema watuhumiwa hao wamekamatwa Jumamosi Aprili 08, 2023 jijini Arusha na kwamba taratibu za mawasiliano ya kisheria ya ndani na ya kimataifa zinaendelea kukamilishwa.

Thabo Bester alitoroka gerezani Mei, 2022 baada ya kuhukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la ubakaji, wizi na mauaji mwaka 2012, lakini polisi wa Afrika Kusini waligundua kutoroka kwake mwezi Machi mwaka huu.

Kenya: Wananchi waacha magari majumbani kutokana na bei kubwa ya mafuta

Awali, alidhaniwa kuwa amefariki katika ajali ya moto iliyotokea gerezani, lakini mwishoni mwa Machi, polisi walisema uchunguzi wa DNA ulibaini kuwa mabaki yaliyopatikana yalikuwa ya mtu mwingine.

Bester amedaiwa kuwarubuni waathiriwa kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook kabla ya kuwabaka na kuwaibia.

Send this to a friend