Aliyoyasema Samatta baada ya kujiunga Fenerbahçe

0
42

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta amejiunga na Klabu ya Fenerbahçe ya Uturuki kwa miaka minne akitokea Aston Villa ya England.

Klabu huyo imemkaribisha nyota huyo na kumtaki kila la heri.

“Najua ukubwa wa klabu ya Fenerbahçe, si tu Uturuki bali duniani kote,” amesema Samatta wakati akizungumza na televisheni ya klabu yake mpya.

Ameongeza kuwa ni mwenye furaha kujiunga na familia hiyo mpya kwa sababu ni fursa na changamoto kubwa kwake.

Amesema kuwa “Fenerbahçe ina mashabiki wengi na mara zote wamekuwa wakitaka ushindi. Mimi pia nataka kushinda. Nina furaha na ninaamini tutashinda mataji mengi.”

Samatta alijiunga Aston Villa Januari 2020 akitokea KRC Genk ya nchini Ubelgiji.

Send this to a friend