Amchoma kisu aliyekuwa mkewe pamoja na mpenzi wake mpya

0
46

Maafisa wa Polisi katika Kijiji cha Muguga, Kaunti ya Kiambu nchini Kenya wamemkamata mwanamume mwenye umri wa miaka 43 ambaye inasemekana alivamia nyumba ya mke wake wa zamani na kumchoma kisu pamoja na mwanaume aliyemkuta ndani ya nyumba hiyo.

Imeelezwa kuwa ni takribani mwezi mmoja tangu wawili hao kuachana na ndipo mpenzi wake huyo wa zamani alipoamua kuhamia kwa mpenzi wake mpya.

Kulingana na walioshuhudia tukio hilo, juhudi za mshukiwa kutoroka ziliambulia patupu baada ya wakaazi kumiminika eneo hilo na kumfungia ndani ya nyumba hadi maafisa wa polisi walipofika na kuwakimbiza waathiriwa hospitalini.

Mwanamke aliyehukumiwa miaka 30 jela kwa kutoitunza vizuri mimba yake aachiwa huru

Kamanda wa Polisi nchini humo, Anthony Mbogo alithibitisha kisa hicho akisema mshukiwa anazuiliwa katika kituo cha polisi na waathiriwa wanapatiwa matibabu.

Send this to a friend