Amteka mtoto wake wa kambo akitaka fedha kutoka kwa mkewe

0
52

Polisi jijini Nairobi nchini Kenya wamemkamata mwanaume anayedaiwa kumteka nyara mtoto wake wa kambo mwenye umri wa miaka 8 ili alipwe pesa na mke wake baada ya ugomvi nyumbani.

Nemwel Ondari (32) alikamatwa saa chache baada ya mama wa mtoto huyo, Everline Nandera kutoa taarifa katika kituo cha polisi baada ya kukuta ujumbe ulioachwa na mume wake akidai fidia ya Ksh 50,000 (TZS 956,316) ili kumuachilia mtoto wake, na kutishia kumuua kwa kisu endapo angekwenda kinyume naye.

Ahukumiwa miaka 5 jela kwa kujirekodi akila popo

Polisi walimfuatilia mtuhumiwa hadi walipompata kwenye stendi ya basi la jiji akiwa amebeba nguo zake pamoja na kisu kwenye mifuko miwili huku akiwa na mvulana huyo.

“Wapelelezi walimvamia mwanamume huyo muda wa saa kumi jioni, huku akingoja kwa shauku pesa hizo kuwekwa kwenye akaunti yake ya simu,” wameeleza polisi.

Polisi wamesema mtuhumiwa kwa sasa anashikiliwa akisubiri kufikishwa mahakamani.

Send this to a friend