Amuua baba mkubwa na mkewe akidai wanamloga

0
49

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema Polisi wanamshikilia Jonas Mushi mkazi wa Manushi wilayani Moshi kwa tuhuma za kumuua baba yake mkubwa pamoja na mkewe (baba mkubwa) kwa kuwakata na panga akiwatuhumu kuwa wanamloga.

Kamanda Maigwa amesema Julai 19 mwaka huu majira ya saa 11 jioni katika kijiji cha Manushi Kati, mtuhumiwa alifika nyumbani kwa marehemu na kuingia ndani kisha akachukua panga na kuanza kumshambulia baba yake mkubwa aitwae Mariki Mushi.

Ameongeza kuwa, wakati akiendelea kumshambulia baba yake mkubwa, mke wa marehemu aitwaye Felister Mushi aliingilia kwa lengo la kumsaidia mumewe asishambuliwe, ndipo mtuhumiwa alimgeukia mama yake mkubwa na kuanza kumshambulia pia hadi walipopoteza maisha.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi.

Send this to a friend