Amuua mke baada ya kumuacha kisha na yeye kujiua

0
50

Watu wawili ambao walikuwa ni mume na mke, wamefariki dunia baada ya mume aliyetambulika kwa jina la Ally Mwakilembe (45) mkazi wa Kijiji cha Kapeta Kata ya Ikinga Wilaya ya Ileje mkoani Songwe kumuua aliyekuwa mke wake, Wema Ndile kwa sababu ya wivu wa kimapenzi.

Jeshi la Polisi mkoani Songwe limesema wawili hao walikuwa wanandoa na walitengana miezi mitano iliyopita, ambapo mke aliamua kwenda kuishi sehemu nyingine ili kuendelea na maisha yake.

Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi, mnamo Oktoba 15, mwaka huu majira ya saa nne na nusu usiku, mwanaume huyo alimshambulia kwa kumchoma kisu mwanamke huyo sehemu za shingoni na ubavuni upande wa kulia akiwa nyumba kwake na kusababisha kifo chake.

Baada ya kutimiza tukio hilo, mwanaume huyo aliamua kujichoma kisu tumboni na kujisababishia majeraha, ambapo alikimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Ileje lakini alipoteza maisha Oktoba 17 alfajiri akiwa anaendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.

Send this to a friend