Amuua mkewe baada ya kuambiwa mtoto si wake

0
55

Mtu mmoja anayefahamika kwa jina Abdallah anatafutwa na Jeshi la Polisi mkoani Pwani kwa tuhuma za kumuua mkewe, Pili Mang’ota (38) mkulima na muuza mbogamboga mkazi wa Sanze, Kata ya Kazimzumbwi wilaya ya Kisarawe.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani humo, Pius Lutumo wakati akizungumza na waandishi wa habari, ameeleza kuwa Abdallah anadaiwa kufanya mauaji hayo baada ya kuambiwa kuwa mtoto wanayemlea si wa kwake.

Sita wakamatwa  kwa kuingiza ng’ombe 2035 Hifadhi ya Tarangire 

Kamanda Lutumo amesema tukio hilo lilifanyika Desemba 17 mwaka huu saa nane mchana ambapo marehemu aliaga nyumbani kuwa anaenda kuchuma mboga shambani na hakurudi tena hadi mwili wake ulipokutwa kichakani ukiwa umefukiwa na kuharibika.

“Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na raia wema walifanikiwa kuupata mwili wa marehemu baada ya kufanya msako ambapo alikutwa akiwa amefariki,” ameeleza Kamanda.

Send this to a friend