Amuua mkewe kisa kapika nyama ya mbuzi wakati hakuacha pesa ya matumizi

0
76

Jeshi la Polisi mkoani Rukwa linamshikilia mwanaume mmoja mkazi wa mtaa wa Chitepo Mazwi, Manispaa ya Sumbawanga kwa kosa la kumuua mke wake, Hawa Suleiman (31) kutokana na wivu wa mapenzi.

Mwanaume huyo ambaye jina lake limehifadhiwa, anadaiwa kuwa alichukizwa na kitendo cha kukuta mke wake amepika nyama ya mbuzi wakati hakumuachia pesa yoyote ya matumizi, na ndipo ugomvi ulipozuka na kuanza kumpiga kwa kutumia kipande cha mti kisha kumkata sehemu za mwili kwa kisu.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) Shadrack Masija amekiri kutokea kwa tukio hilo Oktoba 9, akieleza kuwa mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote pindi upelelezi utakapokamilika.

Akisimulia tukio hilo, mmoja wa majirani, Editha Kawia amesema baada ya mwanaume huyo kurejea nyumbani na kukuta mboga hiyo, mtuhumiwa alimhoji mke wake ni wapi alikopata pesa za kununua nyama na mke wake hakumpa majibu ya kumridhisha.

“Mtuhumiwa alichukua sufuria iliyokuwa na mboga hiyo na kwenda kumwaga nje na ndipo alipotoa shilingi 2,500 na kumpa mke wake ili akanunue mboga nyingine ambayo wataitumia kama kitoweo kwa siku hiyo kisha akaondoka zake,” ameeleza.

Amesema baada ya kurejea baadaye alikuta mke wake amepika dagaa kitu ambacho hakupendezwa nacho akidai hawezi kula dakaa huku akimtishia kumpiga, ndipo mke wake alipokimbia na kurejea nyumbani majira ya jioni, na hapo ndipo ugomvi ulipoanza tena.

Send this to a friend