Amuua mkewe na kuchoma moto kaburi kwa madai ya kuambukizwa UKIMWI

0
35

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo amesema kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo linamshikilia Shaibu Kuselela (58) kwa tuhuma za kumuua mkewe, Amina Mtausi (40) na kumzika kisha kuchoma moto kaburi ili kuficha ushahidi.

Kamanda Katembo amesema kuwa mtuhumiwa alifanya mauaji hayo Februari 28 mwaka huu katika Kijiji cha Lipalwe A Tandahimba, akimtuhumu mkewe kumwambukiza Virusi vya UKIMWI.

“Katika muda na saa isiyojulikana, Kuselela alifanya mauaji ya mkewe kisha akamzika shambani kwao na kuchoma moto kaburi, kisha akatokomea kusikojulikana. Tulipopata taarifa tulifuatilia tukabaini alipo kisha tukamkamata,” amesema Katembo.

Aidha, ameongeza kuwa kabla ya tuhuma hizo, kumbukumbu za mahakama zinaonesha kuwa mwaka 2010 mtuhumiwa aliwahi kufikishwa mahakamani na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kumuua mama yake mzazi bila kukusudia.

Send this to a friend