Amuua mpenzi wake, akatakata viungo na kuvitupa

0
89

Jeshi la Polisi linamshikilia Abdalla Miraji Mussa (42) mkazi wa Sinza kwa Remmy, Dar es Salaam kwa kumuua mwanamke aitwaye Ezania Kamana Mkazi wa Tandika Maghorofani Temeke ambaye anadaiwa kuwa mpenzi wake.

Katika tarifa iliyotolewa na polisi imesema tukio hilo liliripotiwa Agosti 19, mwaka huu ambapo katika uchunguzi zilipatikana taarifa kuwa mwanamke huyo na mtuhumiwa hawakuwa na maelewano mazuri na baada ya kuhojiwa alikataa kuwa hafahamu alipo.

Ameeleza kuwa Agosti 22,2024 zilipokelewa taarifa kuwa katika eneo la Silversand barabara ya mtaa wa Freedom Kunduchi kumeonekana mifuko ambayo ina viungo ambavyo vinadhaniwa ni vya binadamu na baada ya uchunguzi walikuta viungo vya binadamu ambavyo ni paja moja, vipande vya mikono miwili, eneo la kifua, kalio, matumbo na nguo.

“Baada ya kupata viungo hivyo na mtuhumiwa kuelezwa, aliamua kueleza ukweli kuwa alimuua mpenzi wake huyo na kutenganisha mwili wake katika vipande na kwenda kuvitupa maeneo tofauti,” imesema tarifa.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Agosti 23, mwaka huu aliwaongoza askari hadi eneo la Tegeta Block D na kuwaonyesha alipotupa miguu na baadaye aliwaonyesha eneo ambalo alitupa kichwa.

Send this to a friend