Amwagiwa tindikali akidai kugawana mali na mumewe

0
43

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia Lusajo Makiwelu ambaye ni dereva anayedaiwa kuwamwagia tindikali Witness Nguvalwa (31) na mtoto wake wa miezi sita na kuwasababishia maumivu makali.

Akizungumza na Swahili Times Kamanda wa Polisi mkoani humo, Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea Juni 28, mwaka huu wakati mwanamke huyo na mtoto wake wakiwa wanasubiri daladala eneo la Maghorofani jijini humo.

Inadaiwa kuwa mwanamke huyo alifika mkoani humo akitokea mkoani Iringa kuleta wito wa mahakama uliolenga kugawana mali walizochuma pamoja na aliyekuwa mumewe baada ya mahakama kuwatenganisha.

Akamatwa kwa madai ya kuponya UKIMWI kwa kitunguu

Mwanamke huyo aliposhuka kituo cha mabasi Maghorofani alipita mwanaume huyo ambaye hakumfahamu akiwa ameshika kichupa mkononi kilichokuwa na kimiminika kisha kumwagia usoni mara baada ya kuwasalimia.

Polisi wamesema wanamshikilia dereva huyo kama mshukiwa huku mahojiano zaidi yakiendelea.

Send this to a friend