Mtoto mwenye umri wa wiki mbili amefariki dunia baada ya mama yake aliyefahamika kwa jina la Oliva Meshack, mkazi wa Mtaa Buselesele katika mji mdogo wa Katoro wilaya ya Geita mkoani Geita kumzika akiwa hai.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita, Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akieleza kuwa Oliva alifanya kitendo hicho ili apate muda wa kwenda kujiuza.
Padri kizimbani kwa tuhuma za wizi milioni 20
Baada ya kupata taarifa hiyo Kamanda Safia amesema walifukua eneo kilipozikwa kichanga hicho na kukuta tayari amefariki.
Amesema binti huyo ambaye anashikiliwa na polisi mkoani humo alikuwa pia akiuza baa na aliona mtoto huyo angemzuia kuendelea na biashara yake haramu ya kujiuza.