Anastazia ahukumiwa miaka mitatu jela kwa kukutwa na kilo 5 za bangi

0
3

Mahakama ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza imemhukumu Anastazia Mgaya (41) mkazi wa Kijiji cha Mtoni, Kata ya Nakatungu kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kupatikana na dawa za kulevya aina ya bangi kilograms 5.2.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Lucas Nyehega baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri.

Akisoma shtaka hilo, mwendesha mashtaka wa Serikali, Stephen Kabelela ameieleza mahakama kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Machi 03, 2025 huko kata ya katunguru, wilayani humo kinyume na kifungu 17(1)(b) cha Sheria ya dawa za kulevya marejeo ya mwaka 2019.

Aidha, mshatakiwa ameomba apunguziwe adhabu kwakuwa ni mjane na anasumbuliwa na mguu,  hivyo amefanya kosa hilo ili aweze kuitunza familia yake, jambo lililopongwa vikali na mwendesha mashtaka

Send this to a friend