Anayedaiwa kumchoma kisu mpenzi wake asomewa mashitaka akiwa wodini

0
41

Said Selemani (32), mkazi wa Arusha akiwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure, amesomewa shitaka la kumjeruhi mpenzi wake, Faudhia Juma (24) kwa kutumia kisu kisha na yeye kujichana tumboni kwa kisu hicho, kwa madai ya mwanamke huyo kukataa kuolewa naye.

Akisomewa shitaka hilo na Mwendesha Mashtaka Mwandamizi wa Serikali, Martha Mwadenya mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama ya Mkoa wa Mwanza, Stella Kiama, mtuhumiwa ambaye ni Mtaalamu wa Teknolojia ya Habari (IT) amekana kuhusika na tukio hilo.

Mganga mbaroni kwa tuhuma za kuwabaka wanafunzi akidai ni tiba

Aidha, Wakili Mwadenya amesema upelelezi wa kesi hiyo tayari umekamilika, hivyo ameiomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya mshtakiwa kuanza kusomewa maelezo ya awali ya shtaka linalomkabili.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agossti 31 mwaka huu huu itakapoitwa kwa ajili ya kusomwa maelezo ya awali.

Send this to a friend