Anayejiita ‘Yesu’ Kenya akimbilia polisi, wananchi wataka kumsulubisha Pasaka

0
52

Mwanaume wa makamo kutoka kaunti ya Bungoma nchini Kenya, Eliud Wekesa anayejiita Yesu wa Bungoma (Yesu wa Tongaren) amezua mjadala mwingine mtandaoni baada ya kudai kuwa maisha yake yako hatarini.

Kiongozi huyo wa kidini anayefahamika kwa kufanya miujiza na kuiga matendo ya Yesu Kristo akidai ni Yesu halisi aliyerudi, amepeleka madai polisi akidai wakazi wa eneo hilo wanamtishia kumsulubisha kama Yesu Kristo halisi katika Pasaka ijayo wakati ambao Wakristo ulimwenguni wanapoadhimisha kifo na ufufuo wa Masihi.

Madanguro 324 yapo kwenye makazi ya watu Kinondoni

Yesu wa Bungoma amesisitiza kwamba wazo la kumweka msalabani ni uovu, hata kama wakosoaji wake wanashikilia kwamba anapaswa kulipia gharama kama Yesu Kristo halisi ili watu wamuamini.

Madai hayo yameibua hisia nyingi miongoni mwa Wakenya huku wakichangia maoni tofauti kupitia mitandao ya kijamii na wengine wanadai kuwa atafufuka siku ya tatu ikiwa yeye ndiye Yesu.

Yesu wa Bungoma amejizolea umaarufu mkubwa katika miezi ya hivi karibuni kwa mafundisho yake yenye utata na kujitangaza kuwa ni Yesu halisi.

Send this to a friend