Ang’atwa ulimi na mpenzi wake wakijamiiana usiku

0
41

 

Gembe Singu (32) mkazi wa kijiji cha Mwamakalanga  wilayani Shinyanga anadaiwa kung’atwa ulimi na mpenzi wake, Leticia Elias (40) wakati wakijamiiana.

Inadaiwa wapenzi hao walikuwa na ugomvi, na siku ya tukio mwanamke huyo alimuita Singu nyumbani kwake ili wazungumze na kumaliza tofauti zao.

Akisimulia tukio hilo kaka wa kijana huyo, Makoye Singu amedai mkasa huo umetokea Septemba 29, 2022 majira ya saa tatu usiku, na baada ya ndugu yake kupata majeraha hayo walimpeleka hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Shinyanga ili kupatiwa matibabu.

Mwanamke ahukumiwa kifungo cha maisha kwa kubaka mtoto

Ameongeza kuwa hali ya ndugu yake bado si nzuri kwani bado hawezi kuongea vizuri na anakula chakula kwa shida licha ya kuwa anaendelea na matibabu.

Naye Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kubainisha kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi na kwamba upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.

Send this to a friend