Angola yajiondoa kama mpatanishi wa mzozo wa DRC

0
2

Angola imeamua kujiondoa kama mpatanishi katika mzozo unaoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), baada ya kushindwa kufanikisha mazungumzo ya amani kati ya pande zinazohusika.

Taarifa kutoka Ofisi ya Rais imesema Angola inahitaji kujitoa kwenye jukumu hilo ili kujikita zaidi kwenye vipaumbele vya Umoja wa Afrika (AU).

Rais wa Angola na Mwenyekiti AU, Joao Lourenco amekuwa akijaribu kutafuta suluhu ya vita na kupunguza mvutano kati ya DRC na Rwanda, ambayo imekuwa ikishutumiwa kuunga mkono waasi wa M23.

DR Congo na M23 zilipangwa kufanya mazungumzo ya moja kwa moja kwa mara ya kwanza katika mji mkuu wa Angola, Luanda wiki iliyopita baada ya Rais wa Congo Felix Tshisekedi, ambaye kwa muda mrefu alikataa mazungumzo na waasi, kukubali kutuma ujumbe.

Hata hivyo, M23 walijiondoa dakika za mwisho, kufuatia vikwazo vya Umoja wa Ulaya dhidi ya M23 na maafisa wa Rwanda.

 

Send this to a friend