Anjella amshtaki Harmonize BASATA

0
78

Msanii Angelina Samson, maarufu Anjella amewasilisha malalamiko Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), akidai lebo ya Konde Music World Wide inayomilikiwa na msanii Rajab Abdul ‘Harmonize’ iachane naye rasmi.

Madai ya Anjella kuachana na lebo hiyo yamekuja wiki moja baada ya lebo hiyo kumalizana na wasanii wengine wawili Cheed na Killy waliokuwa na malalamiko yanayofanana na hayo.

Kwa mujibu wa gazeti la mwananchi limeripoti kuwa chanzo chao cha kuaminika kimedai kuwa malalamiko ya Anjella ni tofauti na Cheed na Killy, ambapo yeye anadai kupewa barua rasmi ya kuachana naye na kumrudishia digital platform zake na kwamba Novemba Mosi, mwaka huu Harmonize alitakiwa afike Basata kwa ajili ya kusikiliza shauri hilo, lakini hakutokea.

“Mkataba ulikuwa unasema Anjella akiuvunja atawalipa shilingi bilioni moja, lakini wakiuvunja wao watamrudishia ‘digital platform’ zake tu bila hata senti tano, sasa wanachokifanya ni uhuni, wameachana naye kimtindo ila hawataki kumalizana naye kila mmoja ashike njia yake.

“Kama ni fedha za nyimbo zake na lolote likitokea wanaendelea kunufaika wao na si Anjella ambaye wamemuweka kando,” kilisema chanzo hicho cha kuaminika.

Mbali na hilo, inadaiwa kuwa msanii huyo aliahidiwa na Harmonize kusaidiwa matibabu ya mguu jambo ambalo halikufanyika, huku ikielezwa kuwa sababu za Harmonize kutaka kuachana na nae ni pamoja na kutorudisha faida ya kile walichowekeza kwake.

Send this to a friend