Anne Rwigara, mkosoaji wa Serikali ya Rwanda afariki, kifo chaibua utata

0
47

Anne Rwigara (41), aliyekuwa mkosoaji wa Serikali ya Rwanda na mtoto wa mfanyabiashara maarufu wa zamani nchini Rwanda, Assinapol Rwigara amefariki dunia nchini Marekani saa chache baada ya kueleza kupatwa na maumivu makali ya tumbo.

Rwigara alifahamika zaidi baada ya kukamatwa yeye na familia yake na kukaa gerezani kwa siku kadhaa mwaka 2017 baada ya uchaguzi wa urais wakituhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo ukwepaji kodi na kupelekea mali za familia, kikiwemo kiwanda cha tumbaku na akaunti za benki kushikiliwa.

Anne alishtakiwa kwa kosa la kukusudia kusababisha machafuko, kufanya uhalifu alioshirikiana na kaka yake na mama yake na mashtaka mengine na baadaye Anne aliachiliwa na mahakama, lakini dada yake mkubwa Diane, ambaye alitaka kuwania urais, na mama yake Adeline walikaa gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Kwa mujibu wa Reuters, chanzo cha kifo cha mwanamke huyo bado kinatiwa mashaka hadi sasa na watu wa familia yake.

Kifo cha baba yake mwaka 2015, pia kilijawa na utata ambapo familia yake ilidai aliuawa katika ajali iliyopangwa na kumwandikia barua Rais Kagame wakitaka uchunguzi ufanyike juu kifo cha Assinapol.

Send this to a friend