Anusurika kifo baada ya kumeza pete ya uchumba iliyofichwa kwenye chakula

0
56

Kisa kimoja kimetokea nchini Kenya ambapo mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la Jessica Hawayu amenusurika kifo baada ya kumeza pete iliyowekwa kwenye chakula ili kumshangaza (surprise) katika tukio la kuvishwa pete.

Tukio hilo lilifanyika siku ya Jumapili nyumbani  kwa Jesca Gongoni, Kaunti ya Tana River ambapo familia yake pamoja na mpenzi wake waliandaa tafrija ya  kumshtukiza ya kumvisha pete ya uchumba bila yeye kujua.

Wakati akiandaa chakula, mpenzi wake na marafiki zake walikuwa wakizunguka mjini wakisubiri ishara kutoka kwa familia yake mara mambo yatakapokuwa tayari, kisha walipokea ujumbe uliowataka waanze kusogea eneo la tukio majira ya saa mbili usiku.

Mume ajinyonga ukweni baada ya mkewe kugoma kurudi nyumbani

Mpango kati ya mama wa mwanamke huyo na mpenzi wake ulikuwa ni kuifunika pete ya uchumba kwenye sahani ya pilau, ambapo angeigundua wakati akila chakula japokuwa baba yake hakukubaliana na mpango huo.

“Baba alikuwa amepinga wazo hilo lakini kwa kuwa hakukuwa na wazo bora zaidi, tuliamua kulipa nafasi lile tulilokuwa nalo na kuendelea nalo,” amesimulia mmoja wa wanafamilia.

Muda mfupi baada ya kufika eneo la tukio vicheko na shangwe vilizimwa baada ya Jesca kukabwa wakati wa chakula hali iliyopelekea kutafuta namna ya kumuokoa na ndipo baba yake alipompiga mgongoni mara tatu kisha kutapika pete hiyo na kukimbizwa hospitalini.

Send this to a friend