Aokota milioni 13 Makkah, azirudisha kwa mmiliki wake

Mwanamke mmoja kutoka Nigeria, anayefahamika kama Hajiya Zainab amepongezwa kwa kurudisha dola 5,000 [TZS milioni 13.5] alizoziokota katika Msikiti Mtakatifu wa Masjidul Haram, Makkah, na kuzirudisha kwa mmiliki wake raia wa Urusi.
Kwa mujibu wa taarifa, Zainab aliokota pesa hizo muda mfupi baada ya kumaliza kusali, kisha akaamua kuripoti mara moja kwa mamlaka husika.
Tukio hilo limetokea Mei 27, mwaka huu na kuthibitishwa na Tume ya Hija ya Nigeria (NAHCON) pamoja na Bodi ya Mahujaji ya Jimbo la Plateau, inayoongozwa na Daiyabu Dauda.
“Alionyesha uaminifu na maadili ya hali ya juu kwa kurejesha kiasi hicho cha pesa kwa mmiliki halali. Ni tendo la huruma la kipekee,” amesema Dauda.
