Apata faida TZS bilioni 6 kwa kuuza chanjo bandia ya Corona

0
45

China inamshikilia kiongozi wa kundi moja ambaye ametengeneza mamilioni ya fedha kwa kuuza chanjo bandia ya virusi vya corona.

Mtu huyo aliyefahamika kwa jina la Kong inaelezwa kuwa alifanya uchunguzi namna chanjo za corona zinavyofungashwa, kisha akafungasha ‘saline solution na mineral water’ kana kwamba ni chanjo na kufanikiwa kuuza zaidi ya dozi 58,000.

Chanjo hizo feki imeelezwa kuwa zilitoka nje ya nchi lakini haijafahamika zilipekwa eneo gani.

Kong ni miongoni mwa watu 70 ambao wanashikiliwa kwa kosa hilo, ambapo China imeahidi kupambana na wanaokwamisha juhudi za kukabiliana na virusi hivyo.

Mahakama nchini humo imeeleza kuwa Kong na genge lake wametengeneza faida ya Yuan miliomi 18 (TZS bilioni 6.45) kwa kuweka ‘saline solution na mineral water’ kwenye mabomba ya sindano na kuuza kama chanjo ya corona tangu Agosti 2020.

Chanjo hizo zilikuwa zikiuzwa kwa maelezo kuwa zimepatikana kupitia mitandao ya ndani kutoka kwa mtengenezaji halisi.

China ilikuwa imepanga kutoa chanjo kwa watu milioni 100 kabla ya mwaka mpya wa Lunar, wiki iliyopita, lakini imetoa chanjo kwa watu milioni 40. Hata hivyo imefanikiwa kudhibiti maambukizi mapaya kwa kuamuru watu kukaa majumbani, kupima na kufuatilia waathirika.

Send this to a friend