Apigwa shoti akikata nguzo ya umeme kwa shoka

0
74

Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Focus Juma mkazi wa Kijiji cha Nkiniziwa Wilaya ya Nzega, mkoa wa Tabora amekamatwa kwa tuhuma za kukata nguzo ya umeme kwa shoka na kuacha nyaya zikining’inia huku akisababisha baadhi ya vijiji kukosa huduma ya umeme.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mtuhumiwa wakati alipokuwa akitekeleza tukio hilo alipigwa na shoti na kunusurika kifo alipokuwa akikata nguzo inayosafirisha umeme mkubwa wa Kilovolt 132.

WHO kufanya majaribio ya Chanjo ya Ebola nchini Uganda

Baada ya tukio hilo mtuhumiwa alikimbizwa katika kituo cha afya Busondo wilayani Nzega akiwa hajitambui, huku akiwa ameungua katika sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo miguuni, shingoni na mkononi.

TANESCO mkoani Tabora bado wanaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu chanzo cha mtuhumiwa huyo kufanya kitendo hicho.

Send this to a friend